Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Jumuiya ya Walimu wa hawza yaa Qum imelaani msimamo wa upande mmoja wa Al-Azhar ya Misri katika kulinda maslahi ya Marekani na watawala makaimu wa Shetani Mkubwa katika nchi za Ghuba ya Uajemi, na kusema kuwa: “Hii inaonesha kwamba; Al-Azhar haikuweza kutofautisha kati ya upande wa haki na upande wa wakoloni katika mashambulizi ya kigaidi ya Marekani na Israeli. Hali hii imedhoofisha hadhi ya taasisi hii kongwe na haiwezi kurekebishika, na hakika itasababisha upingaji kutoka kwa wale wanaotetea haki."
Jumuiya ya Walimu pia imekumbushia kuwa; Iran daima imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono dhamira ya Palestina, uhuru na heshima ya nchi za Kiislamu, pamoja na kuimarisha umoja wa Kiislamu. Majibu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mashambulizi ya kikatili kutoka kwa wauaji wa watoto Marekani na Israeli ni hatua kamili ya kujihami, na upotoshaji wa ukweli uliofanywa na Al-Azhar unaonesha udhaifu wa uchambuzi wa kisiasa wa taasisi hii ya kidini.
Taarifa Kamili ya Jumuiya ya Walimu wa hawza ya Qum ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu,
Kitendo cha kushangaza na kisicho na mantiki kilichofanywa na Chuo cha Al-Azhar katika kuyalinda kwa nguvu zote maslahi ya Marekani na watawala wa Shetani Mkubwa katika nchi za Ghuba ya Uajemi, ambako nchi hizo zimejitolea kwa utawala wa kibeberu ili taifa la Kiislamu lishambuliwe kijeshi, ni kitendo cha kusikitisha na kilicho na madhara makubwa kwa taasisi hii ya kielimu na kidini.
Kitendo cha kwamba; Al-Azhar haikuweza kutofautisha katika mashambulizi ya kigaidi ya Marekani na Israeli kati ya upande wa haki na wa waliokalia watu kwa nguvu, kimejenga doa kubwa kwa hadhi ya taasisi hii kongwe, na bila shaka, kitawafanya wengi wanaotetea haki kuikosoa.
Majibu ya Iran kwa mashambulizi ya kikatili kutoka kwa Marekani wauwaji wa watoto na Israeli ni hatua ya kujihami, na kushutumiwa kwa Iran na Al-Azhar kunaonesha udhaifu wa uchambuzi wa kisiasa wa taasisi hii ya kidini.
Wataalamu na viongozi wa kidini wa Al-Azhar, kama wanataka kuona uhuru wa Quds iliyo tukufu na kuulinda umma wa Kiislamu kutokana na mgawanyiko na mfarakano, lazima kwanza wamtambue adui mkubwa wa umoja wa umma wa Kiislamu, yaani, Israel na Marekani, na wawe na uelewa wa kutosha kuhusu njama zao.
Iran imekuwa mstari wa mbele katika kuiunga mkono dhamira ya Palestina, uhuru, heshima ya nchi za Kiislamu, na kuimarisha umoja wa Kiislamu, na upotoshaji wa ukweli uliofanywa na Al-Azhar hautaathiri sura ya wema na haki ya Iran, bali utakuwa ni pigo kwa hadhi ya jamii ya Al-Azhar kwenye jamii ya Kiislamu.
Jumuiya ya Walimu wa hawza ya Qum, inaendelea kuutaka umma wa Kiislamu kuwa na umoja na kuepuka migawanyiko, na inasisitiza kuwa; Iran inataka heshima na ustawi kwa majirani zake na nchi za Kiislamu. Heshima hii haiwezi kupatikana isipokuwa kwa kujiepusha na serikali za kibeberu na Shetani Mkubwa, Marekani.
Viongozi na wanazuoni wa jamii ya Kiislamu, hasa wanazuoni wa Al-Azhar duniani kote, wanapaswa kuwa waangalifu kuhusu hila za Marekani na kuzingatia suala la Palestina kama jambo linalo waunganisha.
Israel na Marekani, mbele ya nguvu na ustahimilivu wa Iran, hawawezi kufanikiwa. Kutambua upande wa waathirika na wanaotafuta haki na kusaidia wapiganiaji wa uhuru wa Quds, leo hii ni mtihani mkubwa kwa umma wa Kiislamu, na hakika, watu wa haki na ukweli chini ya msaada wa Mwenyezi Mungu watafanikiwa na kushinda.
Jumuiya ya Walimu wa hawza ya Qum Iran.
Maoni yako